Sunday, March 30, 2014

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein Azindua Barabara Tano Kisiwani Pemba..

Ramani ya Mradi wa ujenzi wa barabara mpya kisiwani Pemba zilizozinduliwa leo na Rais wa Zanzibar Dkt. Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Maofisa wa Ubalozi wa marekani baada ya kuwasili Mtambwe kwa ufunguzi wa barabara tano zilizojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Virginia Blaser, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Barabara mpya tano kisiwani Pemba zenye urefu wa KM 35. uzinduzi huo umefanyika katika moja ya barabara hizo ya Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Virginia Blaser, wakiondoa kipazia kuashiria uzinduzi huo.wa Barabara mpya tano kisiwani Pemba zenye urefu wa KM 35. uzinduzi huo umefanyika katika moja ya barabara hizo ya Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akipanda mti wa historia wakati wa uzinduzi wa barabara ya Mtambwe Pemba.
Kaimu Balozi wa Marekani Nchinin Tanzania akipanda mti wa historia wakati wa uzinduzi wa barabara ya Mtambwe Pemba.